Mtibwa U20 v Dodoma Fc ilikuwa si ya kitoto
Mtibwa U20 v Dodoma Fc ilikuwa si ya kitoto
October 12, 2018
Mabingwa wa kombe la Uhai (U 20 Uhai Cup),Mtibwa Sugar, jana walifanikiwa kucheza mchezo wa kirafiki dhidi ya timu ya Dodoma Fc inayoshiriki ligi daraja la kwanza.
Timu ya vijana chini ya Mtibwa Sugar chini ya kocha Vicent Barnabas jana ilipoteza mchezo wake Wa kirafiki dhidi ya Dodoma 2-1, dakika 45′ za kipindi cha kwanza Dodoma fc iliweza kutawala mchezo na kupata goli 2.
Kipindi cha pili kilianza kwa kasi kwa upande wa Mtibwa Sugar kuweza kumiliki kipindi cha pili na vijana wa wana tam tam walifanikiwa kufunga goli kupitia kwa kiungo wake Abubakar Salum Juma.
Mtandao rasmi wa klabu ya www.mtibwasugar.co.tz umemtafuta kocha wa timu za vijana Vicent Barnabas juu ya mchezo huo wa jana dhidi ya Dodoma Fc.
“vijana wamepoteza kwa timu bora , hii ni mechi ya kirafiki na vijana wamepambana haswaa kiukweli , vijana wamecheza vizuri sana na wengi wao ni wapya nina imani tutaendelea kuwajenga ili kuwa wamoja na kushinda michezo yetu ijayo” Barnabas
Kikosi hicho pia kinakabiliwa na majeruhi ambao ni Abdul Yusuf Haule, Saadun , Joseph Mkuwa Mkele na Omary Sultan ambao wote wanacheza katika nafasi ya ushambuliaji na katika mchezo wa jana hawakujumuishwa.

Post a Comment