Mtibwa yawatandika Mwadui na kushika usukani
Mtibwa yawatandika Mwadui na kushika usukani
September 28, 2018
Wafalme wa soka kutoka mji kasoro bahari, Mtibwa Sugar, jana wamefanikiwa kuibuka na ushindi wa goli 1-0 katika mchezo namba 66 wa ligi kuu bara (Tanzania Premier League), Mtibwa Sugar dhidi ya Mwadui.
Wana tam tam chini ya kocha Zuber Shaaban Katwila walianza mchezo wa jana kwa kasi kubwa sana na walifanikiwa kuandika goli katika kipindi cha kwanza kupitia kwa Stamil Mbonde dakika ya 28′ ya mchezo akipokea pasi kutoka kwa kiungo mshambuliaji Salum Kihimbwa.
Ushindi wa jana unaifanya Mtibwa Sugar kushikilia usukani wa ligi kuu bara (Tanzania Premier League) ikiwa na pointi 13 sawa na MbaoFc ya jijini Mwanza.
Kikosi cha Mtibwa kitaendelea kubakia katika uwanja wake wa nyumbani Manungu kwa ajili ya mchezo ujao dhidi ya Biashara United kutoka mkoani Mara.
Mchezo ujao namba 77 wa ligi kuu bara (Tanzania Premier League) dhidi ya Biashara United utachezwa Jumatatu ijayo ya tarehe 1.10.2018, saa 10:00 jioni, katika uwanja wa Manungu.
Kikosi kilichocheza jana:
Shaaban Kado, Salum Kanoni, Issa Rashid, Hassan Isihaka, Dickson Daud, Shaaban Nditi, Ismail Mhesa, Ally Makarani, Jaffary Kibaya/Ayoub Semtawa, Stamil Mbonde/Henry Joseph, Salum Kihimbwa/Juma Liuzio
Post a Comment